Safe Haven Foundation

CategoriesEvent

Safe Haven Foundation Yagawa Maboksi 100 ya Pedi (Sawa na Pedi 24,000) Kwenda Ofisi Binafsi ya Waziri ya Afya

Safe Haven Foundation Yagawa Maboksi 100 ya Pedi (Sawa na Pedi 24,000) Kwenda Ofisi Binafsi ya Waziri ya Afya kwa ajili ya Watoto wa Kike Wanaoishi Katika Mazingira Magumu Event May 7, 2024 By Safe Haven Foundation Katika kuhakikisha tunawafikia watoto wanaoishi katika mazingira magumu, tulichangia jumla ya boksi 100 za taulo za kike na kuzikabidhi Ofisi Binafsi ya Waziri ya Afya kwa ajili ya kugawiwa kwa watoto wa kike wanaoishi kwenye mazingira magumu. Kupitia ofisi binafsi ya Mheshimiwa Naibu Waziri wa Afya ilikiri kupokea maboksi 100 ya taulo za kike na kuwasilishwa kwa wabunge wa viti maalum katika maeneo husika kwa ajili ya ugawaji. Pia tunapenda kuchukua fursa hii kuishukuru kumshukuru Mheshimkwa Naibu Waziri wa Afya, Dr. Godwin Mollel kwa barua yenye Kumb Na. NWAF/JUM/2024/4 kutushukuru kwa mchango wetu katika kuwasaidia watoto wa kike nchini. Changia (DONATE) SAFE HAVEN FOUNDATION

CategoriesEvent

Safe Haven Foundation Yakabidhi Taulo za Kike 2,400 kwa Wanafunzi wa Kike wa Shule ya Msingi Msimbazi Mseto

Safe Haven Foundation Yakabidhi Taulo za Kike 2,400 kwa Wanafunzi wa Kike wa Shule ya Msingi Msimbazi Mseto Event May 6, 2024 By Safe Haven Foundation Katika kufungua mwezi wa Hedhi Salama ambao ni Mwezi Mei, Safe Haven Foundation tumetembelea Shule ya Msingi Msimbazi Mseto iliyopo katika Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuonana na watoto wakike na kuwaelemisha juu ya Hedhi Salama. Sambamba na hili tumefanikiwa kukakabidhi Taulo za Kike (pedi) 2,400 kwa wanafunzi hao. Tunashukuru kwa wale wote ambao wanaaendela kutuunga mkono katika kufanikisha kuwafikia watoto wengi zaidi. Changia (DONATE) SAFE HAVEN FOUNDATION

CategoriesEvent

Safe Haven Foundation, Samatta Foundation na Uratibu wa Maendeleo ya Uturuki (TiKA) Tanzania Yaadhimisha Miaka 100 ya Jamuhuri ya Uturuki

Safe Haven Foundation, Samatta Foundation na Uratibu wa Maendeleo ya Uturuki (TiKA) Tanzania Yaadhimisha Miaka 100 ya Jamuhuri ya Uturuki Event October 28, 2023 By Safe Haven Foundation Safe Haven Foundation na Samatta Foundation tumeshirikiana na Taasisi ya Ushirikiano na Uratibu wa Maendeleo ya Uturuki (TiKA) Tanzania katika kuadhimisha Miaka 100 ya Jamuhuri ya Uturuki kwa kuzindua ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Miguu wa kisasa katika Shule ya Msingi Msimbazi Mseto. Tunamshukuru Mheshiwa Mkurugenzi wa Halmashauri wa Jiji la Dar es Salaam, Bw. Jomary Satura kwa kukamilisha shughuli kama mgeni rasmi. Changia (DONATE) SAFE HAVEN FOUNDATION

CategoriesEvent

Taasisi ya Safe Haven Yakutana na Mhe. Anjellah Kairuki, Waziri wa TAMISEMI

Taasisi ya Safe Haven Yakutana na Mhe. Anjellah Kairuki, Waziri wa TAMISEMI Event August 22, 2023 By Safe Haven Foundation Taasisi ya Safe Haven imepata nafasi ya kukutana na Mhe. Anjellah Kairuki, Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI). Kukutana na Waziri wa TAMISEMI ni jambo muhimu na lenye manufaa kwetu kama Tasisi.  Tunamshukuru sana Mhe. Anjellah Kairuki kwa ushikiano na mchango wake katika kutuongezea nguvu na kutusaidia ili kufanya zaidi kwa watoto hasa wa kike walio shuleni ili tupate wasomi wa kike wengi zaidi ili waje kunufaisha taifa letu. Changia (DONATE) SAFE HAVEN FOUNDATION

CategoriesEvent

A Visit to the Embassy of the People’s Republic of China in Dar es Salaam, Tanzania

A Visit to the Embassy of the People’s Republic of China in Dar es Salaam, Tanzania Event August 16, 2023 By Safe Haven Foundation Safe Haven Foundation had a meeting with H.E Ambassador Chen Mingjian, Ambassador of the People’s Republic of China in the United Republic of Tanzania. We discussed several issues relating to health and youths, on how we can collaborate with the Embassy of People’s Republic of China in Dar es Salaam, Tanzania. We are grateful for the warm reception of H.E. Ambassador Chen Mingjian.

CategoriesEvent

A Visit To Tuliani Secondary School

A Visit To Tuliani Secondary School Event July 18, 2023 By Safe Haven Foundation Today, 18th July 2023 we manage to visit Turiani Secondary School in Kinondoni, Dar es Salaam to see how they have integrated the girls who had been out of school either due to lack of fees or pregnancies. Turiani is one of the School Centres accommodating the Mama Samia Girls as they are called. We had time to speak to the girls to see from their perspective how coming back to school has been to them. Their approach to being able to advance their education and lives. So far they have 74 Girls who have rejoined the education. At Safe Haven Foundation, we hope to see more students rejoining and advancing their education. The Fund used for this visit was the money donated by Friends of Safe Haven Foundation in Swiss. Changia (DONATE) SAFE HAVEN FOUNDATION

CategoriesEvent

Medical Stores Department (MSD) Donated Drugs Worth Tsh. 1,265,465 to Safe Haven Foundation for Antonia Verna Rehabilitation Centre

On Tuesday, July 4th, 2023, The Non-Governmental Organization of Save Haven Foundation with registration number 00/NGO/R/2963, wrote a letter to the Director General of the Medical Stores Department (MSD) to seek medicines help to the Antonia Verna Community Based Rehabilitation Centre to help 254 children with disabilities related to Autism, Spinal Cord, Cerebral Palsy, Asthma, and Paralysis.

CategoriesEvent

Bohari ya Dawa Tanzania yachangia Dawa Zenye Thamani ya Tsh. 1,265,465 kwa Taasisi ya Safe Haven kwa ajili ya Kituo cha Huduma ya Utengamao cha Antonia Verna

Bohari ya Dawa Tanzania yachangia Dawa Zenye Thamani ya Tsh. 1,265,465 kwa Taasisi ya Safe Haven kwa ajili ya Kituo cha Huduma ya Utengamao cha Antonia Verna Event July 13, 2023 By Safe Haven Foundation Mnamo siku ya Jumanne, 4 Julai, 2023 Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya Save Haven yenye usajili namba 00/NGO/R/2963, iliandika barua kwenda kwa Mkurugenzi Mkuu Bohari ya Dawa (MSD) yenye dhumuni la kuomba msaada wa dawa zinazohitajika katika kituo cha Antonia Verna Community Based Rehabilitation kuwasaidia watoto wenye ulemavu 254, wenye matatizo yanayohusiana na Uti wa Mgongo, Utindio wa Ubongo, Usonji, Kupooza, na Ugonjwa wa Kupooza kwa Ubongo. Antonia Verna Rehabilitation Centre ni kituo ambacho kinahudumia watoto wenye ulemavu na wanatoka katika kaya/familia zinazoishi katika mazingiza magumu kiuchumi kuwahudumia watoto hao. Mnamo tarehe  21 Juni, 2023 tulitembelea kituo hicho cha Huduma ya Utengamao (Rehabilitation Centre) kujionea hali halisi ya kituo na mahitaji wanayohitaji. Kutokana na hali tuliyoiona na mahitaji yanayohitajika ndipo tuliamua kumuandikia barua Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) yenye orodha ya dawa muhimu zinazohitajika katika kituo kuwahudumia watoto wenye uhitaji. Leo Alhamisi 13 Julai, 2023 tuliweza kupokea dawa aina ya Carbamazepine 200mg na Sodium Valproate 500mg zote kwa pamoja zina Jumla ya Shilingi Milioni Moja Laki Mbili Sitini na Tano Elfu na Mia Nne Sitini na Tano (1,265,465/-). Tunapenda kumshukuru Mkurengezi wa Bohari ya Dawa (MSD) pamoja na Wafanyakazi wote kwa Msaada huu walioutoka kuwasaidia Watoto 254 kwa Kituo cha hicho cha Huduma ya Utengamao cha Antonia Verna. Changia (DONATE) SAFE HAVEN FOUNDATION