Katika kufungua mwezi wa Hedhi Salama ambao ni Mwezi Mei, Safe Haven Foundation tumetembelea Shule ya Msingi Msimbazi Mseto iliyopo katika Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuonana na watoto wakike na kuwaelemisha juu ya Hedhi Salama. Sambamba na hili tumefanikiwa kukakabidhi Taulo za Kike (pedi) 2,400 kwa wanafunzi hao.